Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 10:45

Wamarekani waadhimisha siku ya Martin Luther King Jr.


Waziri wa mambo ya ndani wa Marekani Jeh Johnson akiweka shada la maua mbele ya sanamu ya kumbu kumbu ya Martin Luther King, Jr. Jumatatu, Jan. 19, 2015, in Washington. (AP Photo/Jacquelyn Martin)
Waziri wa mambo ya ndani wa Marekani Jeh Johnson akiweka shada la maua mbele ya sanamu ya kumbu kumbu ya Martin Luther King, Jr. Jumatatu, Jan. 19, 2015, in Washington. (AP Photo/Jacquelyn Martin)

Wamarekani kote nchini wanapumzika siku ya Jumatatu ili kuadhimisha sikukuu ya kitaifa kukumbuka siku aliyozaliwa kiongozi mtetezi wa haki za binadamu aliyeuwawa, Martin Luther King Jr.

King alipata umaarufu mwaka wa 1955 alipoongoza mgomo wa kususia mabasi ya umma kwenye mji iliopo kusini wa Montgomery, Alabama na kupelekea kumalizika kwa ubaguzi wa rangi dhidi ya wasafiri weusi. Alikuwa kiongozi mkuu wa harakati za kupigania haki katika miaka ya 50 na 60 huku akiwapa motisha mamilioni ya watu wakati wa hotuba yake ya "I have a dream" kwenye maandamano yaliofanyika machi mwaka wa 1963 hapa mjini Washington Dc.

Aliweza kupata tuzo la Nobel mwaka uliofuata wa 1964 wakati rais Lyndon Johnson alipotia sahihi mswaada wa haki za binadadamu. King aliuwawa tarehe 4 Aprili mwaka wa 1968 huko Memphis, Tennessee alipokuwa amesafiri na kuungana na wafanyakazi weusi wa kuzoa takataka waliokuwa wamegoma wakitaka malipo sawa.

Sikukuu hii ilianza mwaka 1983 wakati rais Ronald Reagan alipotia sahihi mswaada wa kuitenga siku ya Jumatatu ya tatu ya mwezi Januari kuwa ya kumkumbuka King aliyezaliwa Januari 15 ,1929. Congress iliidhinisha sikikukuu ya King kuwa ya kitaifa mwaka 1994 kama siku ya kujitolea katika jamii.

XS
SM
MD
LG