Watu wasiopungua 12 wameuwawa kwenye shambulizi katika ofisi ya jarida la kila wiki la vichekesho Charlie Hebdo, mjini paris Ufaransa Jumatano.
Polisi wa Ufaransa wanasema watu watatu wenye silaha walifyatua risasi katika ofisi za jarida hilo.Washukiwa hao bado hawajulikani walipo.
Mkurugenzi wa jarida hilo Stephanie Charbonnier na wachora katuni watatu waliuwawa . Polisi wawili pia waliripotiwa kuwa ni miongoni mwa waliouwawa.
Jarida hilo la mrengo wa kushoto linafahamika kwa makala yake juu ya dini na utamaduni. Rais Francois Holland wa Ufaransa alilaani shambulio hilo la kigaidi na kutembelea ofisi hizo Jumatano mchana.