Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 27, 2022 Local time: 11:40

Thomas Lubanga ahukumiwa na ICC.


Mbabe wa kivita wa Congo Thomas Lubanga wakati wa kesi yake huko kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC) The Hague, Julai 10, 2012.

Majaji wa mahakama ya rufaa katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu huko Hague wamethibitisha hukumu kifungo cha miaka 14 kwa mbabe wa kivita wa Congo Thomas Lubanga kwa kuhusika kwake katika kuwafunza na kuwaandikisha askari watoto wakati wa mapigano zaidi ya muongo mmoja uliopita katika eneo lenye utajiri wa madini la Ituri huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Lubanga mwenye umri wa miaka 53 hakuonyesha masikitiko yoyote wakati mahakama ilipotoa hukumu hiyo. Amekaa jela kwa miaka minane na anaweza kuachiwa huru mapema baada ya kutumikia theluthi mbili ya hukumu yake. Hiyo ikiwa na maana anaweza kuwa huru mwaka ujao.

Lubanga alishitakiwa kwa kuwateka nyara watoto wadogo wa miaka 11 kutoka majumbani mwao, mashuleni na kwenye viwanja vya mpira na kuwalazimisha kuingia vitani.

Mashirika ya haki za binadamu yanasema kiasi cha raia 60,000 waliuwawa kati ya 1999 na 2006 katika mapigano huko Ituri.

XS
SM
MD
LG