Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 27, 2022 Local time: 07:26

Luteni Kanali Isaac Zida ateuliwa waziri mkuu wa Burkina Faso


Waziri mkuu wa Burkina Faso Luteni Kanali Isaac Zida

Afisa wa cheo cha juu wa jeshi ambaye alikamata madaraka kwa muda mfupi nchini Burkina faso ametajwa waziri mkuu wa serikali ya mpito ya nchi hiyo.

Uteuzi wa Luteni Kanali Isaac Zida ulitangazwa leo, siku moja baada ya rais wa muda Michel Kafando kuapishwa Jumanne mjini Ouagadougou.

Hakuna majibu kutoka Umoja wa Afrika, ambayo ilitishia vikwazo dhidi ya Burkina Faso mpaka Luteni Kanali Zida arejeshe madaraka kwa serikali inayoongozwa kiraia.

Jeshi limemtaja Luteni Kanali Zida mkuu wa nchi hapo Novemba mosi baada ya Rais wa muda mrefu Blaise Compaore kujiuzulu baada ya kukabiliwa na upinzani.

XS
SM
MD
LG