Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 24, 2024 Local time: 02:09

Mvutano mkubwa ndani ya chama tawala cha Zimbabwe ZANU-PF


Wanawake wawiuli wanaohasimiana Zimbabwe mke wa rais Grace Mugabe na makamu raisJoyce Mujuru
Wanawake wawiuli wanaohasimiana Zimbabwe mke wa rais Grace Mugabe na makamu raisJoyce Mujuru

Mke wa rais Robert Mugabe, wa Zimbabwe Bi. Grace Mugabe, amemhimiza mumewe kumfukuza kazi makamu wake Joice Mujuru, ambaye ametuhumiwa kuhusika katika njama ya kutaka kumuuwa kiongozi huyo wa muda mrefu..

Akiwahutubia wanafunzi wa chuo kikuu na wafuasi wa chama tawala cha ZANU-PF katika nyumba yake ya kulea mayatima ya Mazowe siku ya Jumatatu, Bi Mugabe alisema kuwa, mumewe anapaswa kuchukuwa hatua na kumfukuza kazi makamu wake baada ya ripoti kuibuka zinazotuhumu kuwa alikuwa akipanga njama za kumuwa rais huyo wa muda mrefu.

Bi. Mugabe kwa mara kadhaa sasa amemshutumu Bi. Mujuru kwa ulaji rushwa, uzembe wa kazi na kuiuza nchi kwa wanaotaka kuihujumu.

Kufwatia ripoti ilyotolewa Jumapili na gazeti la Sunday Mail, inayomuhusisha Bi. Mujuru na tuhuma za njama za kumuuwa rais, Bi Mugabe aliwashangaza pia wale walohudhuria mkutano wa Jumatatu kwa kusema kuwa ana ushahidi wa kanda ya video inayoonyesha Bi Mujuru akipanga njama za kumuwa yeye mwenyewe, akiongeza kusema kwamba makamu rais anafanya kazi na nchi za kigeni amabazo hazikutajwa katika kutekeleza njama hizo.

Anasema Bi. Mujuru lazima afunguliwe mashtaka ya uhaini.

Kwa upande wake makamu rais Mujuru alizungumza kwa mara ya kwanza kuhusu tuhuma hizo siku ya Jumapili kwa kueleza kwanza mivutano inayoendelea ndani ya chama tawala cha rais Mugabe cha Zanu-PF kabla ya mkutano wake mkuu. Na kukanusha katu ripoti zinazoeleza kwamba anahusika na ulaji rushwa, uzembe na njama ya kutaka kumpindua rais, akisisitiza kwamba hizo ni ripoti za uwongo mtupu.

Bi. Mujuru amesema hamna idadi ya ripoti za uwongo kuhusu yeye, familia yake au washirika wake wa kibiashara zinaweza kumzuia yeye kufanya kazi zake, za kumsaidia Rais Mugabe katika kuendesha miradi ya kijamii na kiuchumi ya serikali hadi ufanisi wake.

Makamu rais anasema yeye yuko tayari kujitetea wakati wowote ule, mbele ya chama cha Zanu PF au kwenye mahakama yeyote ya sheria, kwa mujib wa sheria za Zimbabwe dhidi ya tuhuma zinazotolewa dhidi yake.

XS
SM
MD
LG