Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 28, 2024 Local time: 15:44

Obama aomba bilioni 6 kupambana na Ebola.


Wafanyakazi wa afya wa Guinea wakiwa na nguo za kujikinga katika kituo cha kutibu Ebola karibu na hospitali kuu ya Donka huko Conakry Sept. 25, 2014.
Wafanyakazi wa afya wa Guinea wakiwa na nguo za kujikinga katika kituo cha kutibu Ebola karibu na hospitali kuu ya Donka huko Conakry Sept. 25, 2014.

Rais Barack Obama ameliomba bunge la Marekani kiasi cha dola bilioni 6.18 fedha za dharura ili kupambana na ugonjwa wa Ebola Afrika Magharibi na kuikinga Marekani kutokana na kusambaa kwa ugonjwa huu.

Ombi hilo limetolewa wakati sawa na kutolewa ripoti ya shirika la afya duniani-WHO, Jumanne inayoeleza kwamba kuna watu wachache zaidi walioambukizwa na virusi vya Ebola wiki hii huko Liberia ikiwa ni karibu idadi sawa ya wiki iliyopita huko Guinea na kuongezeka huko Sierra Leonne.

Benki kuu ya Dunia kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa inajaribu kuchangisha kiasi cha dola bilioni moja kwa nchi tatu zinazokumbwa vibaya sana na ugonjwa wa Ebola ambazo ni Guinea, Liberia na Sierra Leonne. Msaada huu wa kifedha unalengo la kusaidia kuharakisha kupelekwa wafanyakazi wa afya wa kigeni kwenye nchi hizo.

XS
SM
MD
LG