Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 25, 2024 Local time: 11:30

Serikali ya Nigeria na Boko Haram wakubali kusitisha mapigano, wakubali kuwaachia wasichana


Watu wanaoandamana na kupiga kelele, wakibeba bango inayosema warudishe wasichana wetu, muda unamalizika, mjini Abuja, Nigeria Sept 11 2014
Watu wanaoandamana na kupiga kelele, wakibeba bango inayosema warudishe wasichana wetu, muda unamalizika, mjini Abuja, Nigeria Sept 11 2014

Kundi la wanamgambo la Boko Haram na serikali ya Nigeria wamefikia makubaliano ya kusitisha mapigano ambayo yanataka kuachiliwa kwa zaidi ya wasichana 200 waliotekwa na wanamgambo hao kutoka mji wa Chibok mwezi April.

Pande hizo mbili zimetangaza makubaliano hayo Ijumaa, baada ya mazungumzo yaliyofanyika nchini Saudi Arabia ambayo yalijumuisha rais wa Chad, Idris Debt na maafisa wa ngazi ya juu kutoka Cameroon.

Hassan Tukur, ambaye ni mshauri wa karibu kwa rais wa Nigeria, Goodluck Nigeria, anasema Boko Haram imechukua hatua ya kwanza ya kuacha chuki.

Bwana Tukur anasema wametangaza sitisho la pekee la kuacha mapigano. Serikali ya Nigeria imejibu na hivi sasa wanafuatilia kuona kama sitisho la mapigano litadumu na ni matumaini yake kuwa litadumu.

Tukur na Danladi Ahmadu, ambaye anajiita mwenyewe kuwa ni katibu mkuu wa Boko Haram, ameiambia VOA kwamba wasichana waliotekwa na kundi la wanamgambo wataachiliwa jumatatu nchini Chad.

Ahmadu amesema wasichana wote wako hai, na kwamba wako katika hali nzuri kiafya na hawajadhuriwa.

Vyanzo vinasema wasichana hao watakabidhiwa kwa rais wa Chad, Idris Deby kwa ajili ya kuwakabidhi kwa maafisa wa Nigeria. Pia wanasema wajumbe wa Nigeria na Boko Haram watakutana katika mji mkuu Chad, Nā€™Djamena, kujadili matakwa ya Boko Haram kama vile kuachiliwa kwa wanamgambo waliofungwa.

ā€‹
XS
SM
MD
LG