Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 20:12

Sudan Kusini karibu kupata amani.


waziri wa mambo ya nje wa Sudan Kusini Barnaba Marial Benjamin,akiwa Juba.
waziri wa mambo ya nje wa Sudan Kusini Barnaba Marial Benjamin,akiwa Juba.

Wapatanishi wanasema pande zinazopingana Sudan Kusini zimepiga hatua ya wastani katika kuunda serikali ya mseto , lakini masuala muhimu yamebaki katika mazungumzo yao ya amani.

Kundi la Afrika Mahariki –IGAD, limesema pande hizo mbili ziliahirisha mazungumzo Jumapili na kupanga kuendelea nayo tena Octoba 16.

Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Kusini Barnaba Maria Benjamin ameiambia sauti ya Amerika mapumziko hayo yanatoa fursa kwa wapatanishi kufanya majadiliano na maafisa .

Mazungumzo ya hivi karibuni yanahusu kuundwa kwa baraza la mawaziri na bunge la mpito ambalo serikali itakuwa nalo pamoja na mkakati wa kutatua mizozo.

IGAD imesema masuala yaliyobaki yatahitaji uamuzi madhubuti kutoka kwa viongozi wa pande zote. Pia wameeleza kuvunjwa moyo kutokana na ukiukwaji wa makubaliano ya sitisho la mapigano ikisema kuwa chaguo la vita lazima litupiliwe mbali.

Wapatanishi pia walisihi pande zote kuruhusu misaada ya kibinadamu kufikiwa wenye mahitaji.

XS
SM
MD
LG