Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Septemba 09, 2024 Local time: 22:01

Rais wa Zambia ashindwa kuhutubia baraza la UN.


Rais Mpya wa Zambia Michael Sata alipoapishwa mjini Lusaka, Septemba 23, 2011.
Rais Mpya wa Zambia Michael Sata alipoapishwa mjini Lusaka, Septemba 23, 2011.

Rais wa zambia Michael Satta amelazwa hospitali mjini New York. Bwana Sata alikuwa New York kuhudhuria mkutano wa mwaka wa viongozi wa dunia katika baraza kuu la umoja wa mataifa ambapo alitakiwa kutoa hotuba yake Alhamisi.

Hakuweza kutoa hotuba hiyo kwa wanachama 193 wa taasisi hiyo ya dunia. Ofisi ya habari katika idara ya polisi mjini New York imewaambia waandishi wa habari alipelekwa hospitali Alhamisi lakini haikutoa maelezo zaidi kuhusu ni hospitali gani wala hali ya bwana Sata.

Ofisi hiyo imethibitisha ripoti kwamba madaktari wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani walimtibu bwana Sata mapema siku hiyo katika hoteli.

Rais huyo mwenye umri wa miaka 77 hajaonekana hadharani kwa takriban miezi mitatu kabla ya kuhudhuria ufunguzi wa bunge la Zambia wiki iliyopita.

Mwanzoni mwa hotuba yake mjini Lusaka, bwana sata aliwaambia wabunge kwa utani “ bado sijafa.” Wasiwasi kuhusu afya ya bwana Sata uliongozeka nchini Zambia tangu aliposafiri kwenda Israel kwa matibabu mwezi juni na baadae kujiondoa kwenye macho ya umma.

XS
SM
MD
LG