Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 23:04

Mataifa ya Kiarabu yaungana na Marekani dhidi ya ISIS


Maeneo yanaoshikiliwa na kundi la Islamic State huko Irak na Syria
Maeneo yanaoshikiliwa na kundi la Islamic State huko Irak na Syria

Mataifa 11 ya kiarabu yamekubaliana na Marekani kuratibu na kushirikiana katika vita dhidi ya kundi la wanamgambo wa kislamu la Islamic State, IS huko Iraq na Syria.

Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa baada ya mkutano ulofanyika Jeddah, Saudi Arabia siku ya Alhamisi, washirika wa Marekani huko Mashariki ya Kati waliahidi kutoa mchango wao unaohitajika katika vita vya pamoja dhidi ya IS, na kueleza kwamba watajiunga katika sehemu mbali mbali za mkakati wa kijeshi ikihitajika.

Msimamo huo ulichukuliwa baada ya waziri wa mambo ya nchi za nje John Kerry kukutana huko Jeddah na mawaziri wa mataifa sita wa Baraza la Ushirikiano wa Ghuba (Saudi Arabia, Kuwait, Bahrain, Qatar, Oman na Umoja wa Falme za Kiarabu), pamoja na Misri, Irak, Jordan na Lebanon.

Mataifa hayo yalikubali kuzuia wapiganaji wa kigeni kupita katika nchi zao, kupambana na wanaogharimia Islami State na makundi mengine ya siasa kali na kusaidia juhudi za huduma za dharura.

Katika hotuba yake kwa taifa siku ya Jumatano usiku , Rais Barack Obama alisema anapanua mashambulizi dhidi ya wanamgambo wa IS na hatosita kuamrisha mashambulizi dhidi ya wanamgambo huko Syria.

please wait

No media source currently available

0:00 0:06:30 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Viongozi wengi wa nchi za kiarabu wameunga mkono mkakati wa Rais Obama wa kuanza mashambulizi ya kukiangamiza kikundi la Islamic State.

Hata hivyo Iran inaeleza kwamba inahitaji Marekani ifafanuwe zaidi juu ya mkakati huo na serikali ya Syria inasema shambulio lolote ndani ya ardhi yake itahitaji ushirikiano na Damuscus.

XS
SM
MD
LG