Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 05, 2024 Local time: 06:39

Hali yazidi kuzorota Fergusson Missouri.


Polisi akiwa kwenye gari la kujilinda anaangalia wakati mabomu ya machozi yakirushwa kusambaza wananchi.
Polisi akiwa kwenye gari la kujilinda anaangalia wakati mabomu ya machozi yakirushwa kusambaza wananchi.

Gavana wa jimbo la Missouri nchini Marekani ameamrisha jeshi la akiba la ulinzi wa taifa kwenda katika mji wa Ferguson baada ya wiki moja maandamano ya ghasia yaliyosababishwa upigaji risasi wa kijana mmoja Mmarekani mweusi na afisa wa polisi mzungu.

Jumapili usiku polisi wakiwa na nguo maalum za kuzuia risasi na kofia za kuzuia gesi walirusha mabomu ya machozi kutawanya kundi la watu waliokuwa wakiandamana kuwafuata polisi hao.

Polisi wanasema baadhi ya waandamanaji walishambulia polisi kwa moto na kuwafyatulia risasi na kujiingiza katika vitendo vya kupora na kuharibu mali lakini hakuna polisi walioripotiwa kujeruhuiwa.

Polisi walielezea ghasia hizo kama vitendo vya jinai vilivyopangwa mapema na vilivyolenga kuharibu mali , kuumiza watu na kuchokoza majibu ya polisi. Watu kadhaa walijeruhiwa.

XS
SM
MD
LG