Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 18, 2025 Local time: 13:19

Marekani yaeleza athari za mashambulizi Iraq.


Mwanamke mmoja kutoka kabila la wachache la Yazidi , ambao amekimbia ghasia katika mji wa Sinjar, Agosti 14, 2014.
Mwanamke mmoja kutoka kabila la wachache la Yazidi , ambao amekimbia ghasia katika mji wa Sinjar, Agosti 14, 2014.

Wizara ya ulinzi ya Marekani inasema operesheni ya kuokoa wakimbizi kutoka mlimani huko kaskazini mwa Iraq huenda isifanyike baada ya uchunguzi kugundua kuwa kuna wakimbizi wachache katika eneo hilo kuliko ilivyofikiriwa hapo awali.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Chuck Hagel akizungumza na waandishi wa habari Jumatano Usiku, alielezea athari za mashambulizi ya anga dhidi ya kundi la Islamic State na kuangusha kwa njia ya anga misaada ya kibinadamu katika kusaidia kuboresha hali katika mlima Sinjar.

Wakurdi wa Iraq na makabila mengine ya walio wachache walikimbilia mlima Sinjar kabla ya shambulizi baya la wanamgambo katika eneo hilo kubwa karibu na mpaka wa Syria.

Wakati huo huo waziri mkuu wa Iraq aliye matatani Nouri al Maliki amekataa wito wa msukumo unaoongezeka wa jumuiya ya kimataifa kumtaka ajiuzulu. Bw. Maliki mwenye nia ya kuhudumu kwa muhula wa tatu alisema jumatano kwamba hataachia madaraka mpaka mahakama ya serikali kuu itoe uamuzi juu ya maamuzi ya rais mpya Fouad Massoum kumteuwa mpinzani wa Maliki kuwa waziri mkuu.

XS
SM
MD
LG