Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 19:48

Ukawa watishia kufanya maandamano Tanzania.


Wabunge ndani ya bunge la Tanzania mjini Dodoma.
Wabunge ndani ya bunge la Tanzania mjini Dodoma.

Nchini Tanzania viongozi wanaounda kundi la umoja wa katiba ya wananchi- UKAWA wametishia kufanya maandamano ya nchi nzima iwapo Rais Jakaya Kikwete hatasitisha vikao vya bunge maalum la katiba vinavyoendelea hivi sasa.

Viongozi hao James Mbatia wa NCCR MAGEUZI, Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF na Freeman Mbowe wa CHADEMA wamesema UKAWA inaamini kwamba hakuna katiba itakayotengenezwa kwa kudharau maoni ya wananchi na bila kuwa na maridhiano hivyo kuendelea na bunge maalum la katiba ni kupoteza fedha nyingi za walipa kodi.

James Mbatia amesoma azimio hilo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam Jumatano.

Kiongozi mwingine wa UKAWA Profesa Ibrahim Lipumba amesisitiza kwamba Rais alifanya kosa kubwa kuvunja iliyokuwa tume ya mabadiliko ya katiba kabla ya kumalizika kwa mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya huku Mwenyekiti wa CHADEMA taifa , Freeman Mbowe akilalamikia alichodai kuyumba kwa uongozi wa nchi katika kipindi hiki muhimu kwa mustakbali wa taifa.

Kundi la UKAWA linalojumuisha wanachama wa vyama vya siasa vya upinzani vimesusia vikao vya bunge maalum la katiba tangu kuanza tena kwa vikao hivyo Agosti tano mwaka huu kwa madai kwamba rasimu ya katiba inayojadiliwa sio iliyopelekwa bungeni na iliyokuwa tume ya mabadiliko ya katiba mgogoro mkubwa ukiwa kwenye muundo wa muungano wa Tanganyika na Zanzibar

XS
SM
MD
LG