Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 20:22

Malaysia yapokea kisanduku cha ndege ya MH 17.


Mpiganaji anayeunga mkono Russia akikabidhi kifaa cha taarifa ya ndege kutoka ndege ya Malaysia nambari 17 katika mji wa Donetsk, mashariki mwa Ukraine, Julai 22, 2014.
Mpiganaji anayeunga mkono Russia akikabidhi kifaa cha taarifa ya ndege kutoka ndege ya Malaysia nambari 17 katika mji wa Donetsk, mashariki mwa Ukraine, Julai 22, 2014.

Waasi wanaounga mkono Russia wamekabidhi taarifa za ndege ya Malaysia iliyoanguka kwa wataalam wa nchi hiyo ikiwa ni pamoja na kisanduku kinachohifadhi taarifa za safari za ndege.

Makabidhiano hayo yalitokea Jumatatu usiku katika mji wa mashariki wa Ukraine wa Donetsk. Yalitokea muda mfupi baada ya waziri mkuu wa Malaysia Najib Razak kuzungumza kwa njia ya simu na kiongozi wa waasi Alexander Borodai.

Kanal wa Malaysia Mohamed Sakri amesema masanduku hayo yalikuwa yameharibiwa kwa kiasi fulani lakini bado yalikuwa katika hali nzuri.

Wakati huo huo, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, jana lilikubaliana kwa kauli moja kuwa makundi yenye silaha yanayodhibiti eneo lililotunguliwa ndege ya Malaysia nambari 17, waruhusu wakaguzi kuingia eneo hilo bila masharti.

Baraza hilo lilishutumu vikali kitendo cha kutungua ndege hiyo na kutoa mwito uchunguzi wa kina ufanywe na wapelelezi wa kibinafsi kutoka jumuiya ya kimataifa.

XS
SM
MD
LG