Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 25, 2022 Local time: 20:03

Israel aahidi kuongeza mashambulizi Gaza.


Mashambulizi ya Israel dhidi ya Hamas.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anasema jeshi la nchi yake litaongeza mashambulizi yake huko Gaza baada ya wanamgambo wa Hamas kukataa pendekezo la kusitisha mapigano na kuendelea kufyatua roketi ndani ya Israel.

Bw.Netanyahu amesema jumatatu kwamba angependa kusulisha mzozo huo kwa njia ya kidiplomasia lakini vitendo vya Hamas havimpi nafasi yeyote bali kupanua na kuongeza kampeni dhidi yao.

Jeshi la Israel lilisitisha mashambulzi kwa saa sita baada ya kukubaliana na mpango wa Misri wa kusitisha mapigano jumatatu asubuhi. Lakini Israel inasema imeanza tena mashambulizi ya anga baada ya wanamgambo kurusha kiasi cha roketi 50 kuelekea Israel kutoka eneo lililodhibitiwa na Hamas.

Maafisa wa Hamas mapema jumatatu walieleza kwamba hawajachukua uamuzi bado lakini tawi la kijeshi la kundi hilo lilikataa pendekezo na Misri likidai kwamba itakua ni kujisalimisha.

XS
SM
MD
LG