Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 08:52

Marekani yasheherekea Uhuru wake.


Eneo la Brooklyn Borough Hall ambapo bendera kubwa ya Marekani imetundikwa alhamisi , July 3, 2014.
Eneo la Brooklyn Borough Hall ambapo bendera kubwa ya Marekani imetundikwa alhamisi , July 3, 2014.

Kote nchini Marekani Ijumaa wanasherehekea miaka 238 ya uhuru kutoka kwa Waingereza, kwa magwaride, pikniki, fataki na matamasha.

Sherehe za siku ya Uhuru mjini Washington Dc zinajumuisha waigizaji mbali mbali wakiwakumbuka na kuwaelezea marais wa zamani Thomas Jefferson, Benjamin Franklin na John Adams.

Kutakuwa na tamasha pamoja na fataki kwenye uwanja wa kitaifa Ijumaa usiku.Tamasha hilo litakuwa na wanamuziki Frankie Valli,Patti Labelle, Michael Donald , Muppets na bendi ya taifa ya Symphony.

Hata hivyo hali ya hewa inaweza kuharibu mipango ya mamilioni ya wamarekani wakati kimbunga Arthur kikisafiri kuelekea pwani ya mashariki.

XS
SM
MD
LG