Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 10, 2022 Local time: 08:22

Mbunge wa Somalia auwawa katika shambulizi.


Mtu mmoja akipekua mabaki katika shambulizi la sokoni huko Hamaerweyne wilaya ya kusini mwa Mogadishu January 26, 2012. REUTERS/Feisal Omar (SOMALIA - Tags: DISASTER ENVIRONMENT BUSINESS)

Mbunge mmoja wa Somalia ameuwawa katika shambulizi la bunduki linalodaiwa kufanywa na kundi la wanamgambo wa Alshabab.

Mohamed Mahmud Hayd aliuwawa alhamisi wakati mtu mwenye silaha alipofyatulia gari lake risasi katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu.

Mbunge mwingine aliyekuwa naye kwenye gari Abdullahi Ahmed Conka aliiambia sauti ya Amerika kwamba washambuliaji hao waliendesha gari lao karibu yake na kufyatua risasi. Anasema mlinzi wa Hayd alijibu kwa risasi lakini aliuwawa pia.

Afisa mmoja wa bunge kwenye gari hilo alijeruhiwa wakati Conka alinusurika bila kuumia .

Al-Shabab yenye mahusiano na Alqaeda ilidai haraka kuhusika na mauaji hayo.

XS
SM
MD
LG