Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 18, 2024 Local time: 03:52

Nchi za Afrika mashariki zawasilisha bajeti.


Marais watatu wa Afrika mashariki Uhuru Kenyatta wa Kenya, Yoweri Museveni wa Uganda na Paul Kagame wa Rwanda huko Kampala, Juni 25, 2013.
Marais watatu wa Afrika mashariki Uhuru Kenyatta wa Kenya, Yoweri Museveni wa Uganda na Paul Kagame wa Rwanda huko Kampala, Juni 25, 2013.
Serikali za Kenya, Tanzania, Rwanda na Uganda zimewasilisha bajeti za mwaka wa fedha wa 2014/15 kila nchi ikilenga katika kuboresha maendeleo ya uchumi na kupunguza kiwango cha umaskini.

Huko nchini Kenya, serikali imetangaza bajeti ambayo inalenga Zaidi katika kuboresha ulinzi wa taifa, elimu, afya, mawasiliano ya reli na barabara pamoja na kilimo.
Bajeti ya Kenya katika mwaka huu wa fedha imeonekana ina unafuu kwa mwananchi wa kawaida kwa vile serikali haikuongeza bei za bidhaa muhimu, lakini imesisitiza utoaji wa mikopo kwa vijana.

Katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2014/15 serikali ya Tanzania ina azma ya kupandisha mishahara ya watumishi wa umma na kupunguza kiwango cha tozo ya kodi ya mishahara kutoka asilimia 13 hadi asilimia 12.

Kama ilivyotarajiwa na wengi nchini humo serikali imeongeza kodi kwa bidhaa mbali mbali, ikiwemo vinywaji vikali, sigara, bia, soda na mvinyo, na bei ya bia inayotengenezwa nchini imepandishwa bei.

Serikali ya Rwanda imewasilisha bajeti ambayo inasadikiwa kuwa inamlenga zaidi mwananchi wa kawaida kinyume na bajeti zilizopita, na mkakati ukiwa ni kuwapunguzia wananchi umaskini na kuwaondoa katika kundi la ufukara.

Bajeti ya Uganda imelenga zaidi katika kuongeza ushuru katika bidhaa mbali mbali ili kuongeza mapato ya serikali na wakati huo huo ikibuni njia za kupunguza utegemezi wa mataifa fadhili.
XS
SM
MD
LG