Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 00:08

Hatimae Al-Sissi atangaza atagombania kiti cha rais Misri.


Mkuu wa zamani wa Jeshi la Misri na aliyekuwa waziri wa Ulinzi Abdel Fattah al-Sisi alipotoa hotuba kwenye televisheni. July 3, 2013. (AFP/Egyptian TV)
Mkuu wa zamani wa Jeshi la Misri na aliyekuwa waziri wa Ulinzi Abdel Fattah al-Sisi alipotoa hotuba kwenye televisheni. July 3, 2013. (AFP/Egyptian TV)
Waziri wa ulinzi wa misri na mkuu wa jeshi Abdel Fatahh al-Sissi ametangaza katika hotuba kwa taifa kupitia televisheni Jumatano kwamba anajiuzulu kutoka wadhifa wake wa waziri wa ulinzi na kugombania kiti cha rais katika uchaguzi ujao unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao. Tangazo hilo linafikisha kikomo wiki kadhaa za uvumi kwamba ana mipango ya kugombania nafasi hiyo.

Field Marshal Sissi anasema anajiuzulu kama waziri wa ulinzi na anagombania kiti cha rais katika tangazo kwenye kwenye televisheni ya taifa, baada ya kukutana na baraza kuu la majeshi ya taifa akiwemo kaimu rais Adly Mansour.

Anasema kwamba anajitokeza kwa mara ya mwisho katika mavazi ya kijeshi baada ya miaka 45 ya kulihudumia taifa, lakini anasema ataendelea kulilinda taifa katika jukumu jipya. Alisema hakuna anayeweza kuwa rais dhidi ya matakwa ya wananchi na bila ya uungaji mkono wao, kama ilivyokua enzi za zamani.

Tangazo hilo halikuwashangaza wengi kwani kulikuwepo na uvumi wa wiki kadhaa kwamba Jenerali Sissi atagombania kiti cha rais. Katika hotuba yake alitoa wito kwa wamisri kumuunga mkono katika juhudi zake kugombania nafasi kuu hiyo ya taifa.

Jenerali alisema wamisri wanahaki ya kuishi kwa hadhi na uhuru lakini ni lazima kila mtu afanye kazi na kuzalisha matunda kuiweka Misri katika nafasi yake inayostahiki miongoni mwa mataifa yenye ustaarabu. Vile vile alisema Misri ni taifa wa wakazi wake wote na hakuna yeyote anayebidi kutengwa.

Tangazo lilitolewa kukiwepo na mapambano ya hapa na pale kati ya polisi na wanafunzi wanaounga mkono kundi lililopigwa marufuku la Muslim Brotherhood katika chuo kikuu cha Cairo na maeneo mengine kadhaa ya mji mkuu huo. Polisi walifyatua mabomu ya kutoa machozi wakazi wa jioni na kuna ripoti za watu kadhaa waliojeruhiwa.

Wafuasi wa Jenerali Sissi walikusanyika katika maeneo kadhaa ya mji mkuu wakati fashasha zilifyatuliwa kwa kutarajia kutangazwa kwamba anagombania kiti cha rais.

Baraza la mawaziri la Misri linatarajiwa kukutana Alhamisi asubuhi kumteuwa mtu atakaye chukua nafasi ya Jenerali. Vituo vya televisheni za setalaiti vya kiarabu vimeripoti kwamba Jenerali mkongwe Sobhi Sudqi amepandishwa cheo na atachukua nafasi ya Jenerali Sissi.

Waziri mkuu Ibrahim Mehleb amesema serikali yake itabaki na msimamo wa kutopendelea upande wowote katika utaratibu wa uchaguzi.

Kundi la Muslim brother hood katika ukurasa wake wa tovuti kwamba kujitangaza mgombea kiti cha rais kunamaanisha Jenerali Sissi alipanga njama ya kumpindua rais Mohamed Morsi .
XS
SM
MD
LG