Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 14, 2024 Local time: 17:42

Mapigano yazuka tena Sudan Kusini.


Wapiganaji wa upande wa jeshi la serikali Sudan Kusini.
Wapiganaji wa upande wa jeshi la serikali Sudan Kusini.
Mapigano mapya yamezuka Sudan kusini, na hivyo kutishia sitisho la mapigano kati ya serikali na waasi ambalo lilifikiwa mwezi uliopita. jeshi la sudan kusini linasema waasi wameshambulia maeneo ya serikali leo asubuhi huko Malakal, mji mkuu wa jimbo linalozalisha mafuta la Upper nile.

Msemaji wa majeshi ya waasi, Lul Ruai Koang ameiambia Sauti ya Amerika (VOA) kuwa waasi walikuwa wanajibu mashambulizi ya serikali. Waasi hao wanasema wamechukua udhibiti kamili wa mji, ambao waliukamata hapo kabla.

Msemaji wa jeshi anasema waasi wamekamata sehemu ya mji. Katika ujumbe wa twitter, Toby Lanzer afisa wa juu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa kwa Sudan kusini, amezisihi pande zote kuheshimu haki za watu na kuwalinda raia.
XS
SM
MD
LG