Mlipua mabomu wa kujitoa muhanga ameuwa watu wapatao 5 katika makao makuu ya Polisi katika mji mkuu wa Misri, Cairo, mabomu matatu ya kwanza kupiga mji huo mapema Ijumaa.
Maafisa wa usalama wanasema mshambuliaji huyo alijilipua kwenye eneo la kuegesha magari la kati kati ya mji katika mashambulizi makubwa nchini humo katika miezi kadhaa.
Saa chache baadaye maafisa wanasema mlipuko mwingine karibu na kituo cha treni upande wa pili wa mto Nile uliua mtu mmoja na kujeruhi wengine kadhaa.
Wizara ya mambo ya ndani inasema shambulizi la tatu lilitokea huko Giza karibu na kituo cha Polisi kwenye bara bara kuu iendayo kwenye mapyramid lakini hakukuwa na majeruhi.