Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 28, 2025 Local time: 12:46

Walinda amani wauwawa Sudan.


 Walinda amani kutoka Senegal na Jordan wauwawa.
Walinda amani kutoka Senegal na Jordan wauwawa.
Umoja wa mataifa unasema walinda amani wawili wameuwawa wakati wakifanya doria katika eneo lenye mzozo la Darfur Sudan.

Afisa mmoja wa Jordan na mlinda amani kutoka Senegal waliuwawa wakati msafara wao uliposhambuliwa na watu wasiojulikana wenye silaha jana Jumapili.

Zaidi ya wanajeshi 12 wa kimataifa kutoka kwenye mpango wa kulinda amani wa umoja wa Afrika wameuwawa huko Darfur katika miezi mitano iliyopita.

Eneo la magharibi la Sudan limegubikwa na ghasia tangu mwaka 2003 wakati waasi walipochukua silaha dhidi ya serikali huko Khartoum wakiishutumu kwa kutengwa.
XS
SM
MD
LG