Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 14:19

Watu wasiojulikana wachoma ofisi za Chadema Arusha.


Mkutano wa chama cha upinzani cha Chadema kumaliza kampeni za uchaguzi wa 2010 Dar es Salaam.
Mkutano wa chama cha upinzani cha Chadema kumaliza kampeni za uchaguzi wa 2010 Dar es Salaam.
Wimbi la mtikisiko linaendelea kukumba chama cha upinzani cha Chadema nchini Tanzania ambapo mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Singida Bw.Wilfred Noeli Kitundu ametangaza kujiuzulu kufuatia kutoafiki maamuzi ya kamati kuu ya chama hicho ya kuwavua madaraka aliyekuwa naibu katibu mkuu Bw. Zitto Kabwe na mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Arusha Samson Mwigamba na mjumbe wa kamati kuu Dr. Mkumbo Kitila .

Wakati huo huo, mkoani Arusha watu wasiojulikana wameshutumiwa kuchoma moto ofisi za chama cha hicho Jumanne asubuhi na kusababisha uharibifu mdogo.
Akizungumza na Sauti ya Amerika katibu wa Chadema mkoa wa Arusha Bw. Amani Golugwa amesema watu hao walijaribu kuingia chumba cha kompyuta chenye taarifa zao zote kuwasha moto huo lakini walishindwa hivyo wakaamua kusababisha shoti ya umeme ambayo ilisababisha moto ambao uliunguza bafu na choo na eneo la paa.
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:52 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Kuhusu nani wanahusika amesema ni mapema mno kusema sababu ya uchunguzi bado unaendelea lakini ameongeza kuwa tukio hilo limewafedhehesha na limewashtua sana akiongeza kwamba kitengo cha upelelezi wa ndani ya chama inafanya kazi na itashirikiana na jeshi la polisi ambalo limechukua alama za vidole za washukiwa katika eneo la tukio.

Kuhusu viashiria amesema vipo kwasababu chama chao kinajisafisha na ukweli ni kwamba chama hicho kinatumbua majipu ingawa watu wengine wanaweza kutafsiri ni mgogoro ndani ya chama ni kwamba “bundi” ametua Chadema na “bundi” amefukuzwa na kwa uzoefu wake anaamini kwamba zoezi lao la kushughulikia “wahaini na wasaliti katika chama hicho linaweza kuwa la maumivu kwa wale waliokuwa na nia mbaya na malengo ndani ya Chadema kwa sababu mpango wao umeshindwa.”
XS
SM
MD
LG