Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 03, 2024 Local time: 15:47

Viongozi Afghanistan wafikiria kuunga mkono mpango wa usalama wa Marekani.


Rais wa Afghanistan Hamid Karzai akizungumza katika siku ya kwanza ya bunge huko Kabul, Nov. 21, 2013.
Rais wa Afghanistan Hamid Karzai akizungumza katika siku ya kwanza ya bunge huko Kabul, Nov. 21, 2013.
Rais wa Afghanistan amesema anaunga mkono makubaliano ya pande mbili ya usalama yaliofikiwa na Marekani ambayo yataacha majeshi ya Marekani huko Afghanistan mpaka 2024 na pengine zaidi.

Lakini ameongeza kuwa pengine mpango huo hautasainiwa mpaka raia wa Afghanistan watakapochagua rais mpya mwezi Aprili.

Katika hotuba iliyokuwa na hisia kali kwa viongozi wa kikabila 2500 rais wa Afghanistan Hamid Karzai alitetea makubaliano ya pande mbili ya usalama yaliofikiwa na Washington akisema kwamba yatawafaidisha raia wa Afghanistan katika muda mrefu ujao.

Akisema alikuwa na uungaji mkono washirika wakuu wa Afghanistan na majirani isipokuwa Iran Bw.Karzai alilitaka bunge lijulikanalo kama Loya Jirga kuupigia kura mpango huo wa usalama.

Lakini katika kile kinachoweza kuwa jambo muhimu na Marekani , Bw.Karzai amesema ikiwa Jirga wataidhinisha waraka huo na bunge la Afghanistan likapiga kura kuunga mkono mpango huo,”makubaliano hayo huenda yakasainiwa baada ya uchaguzi wa rais wa 2014.
XS
SM
MD
LG