Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 16:55

Watanzania wana utamaduni wa kutotaka kulipa kodi-Masala.


TRA
TRA
Hali katika eneo maarufu la biashara la Kariakoo jijini Dar es Salaam Tanzania imeendelea kuwa siyo ya kawaida baada ya wafanyabiashara kufunga maduka yao hapo jana kutokana na wafanyabiashara hao kugoma kutumia mashine za kieletroniki (EFD), ambazo wamelazimishwa kuzitumia ili kudhibiti ulipaji kodi nchini humo.
Akizungumza na Sauti ya Amerika Kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya mapato nchini Tanzania Bi .Diana Masala ambaye ameeleza pamoja na bei kubwa ya mashine hizo kuwa zina faida zaidi kwa wafanyabiashara na uchumi wa Tanzania kwa ujumla.
Amesema mashine hizo zimetengenezwa kulingana na mahitaji ya Tanzania na unaingiza bidhaa zako zote ulizonunua ukiuza inajulikana kabisa umeuza kiasi gani na imebaki kiasi gani tofauti na za mwanzo ambazo hazikuwapa matarajio waliyokuwa wakitegemea kwasababu zilitoa risiti tu na haikuweka kumbu kumbu yeyote, kwa hiyo hawakuweza kujua biashara inakwendaje na uchumi wa nchi kwa ujumla.
Kuhusu kuelimisha wafanya biashara ameeleza kuwa walifanya kampeni na waandishi wa habari, wafanya biashara wa sekta mbali mbali kama vile wafanyabiashara wa spea za magari, ujenzi n.k.
Na pia walipita kila mahali jijini Dar es Salaam, Ilala, Temeke na Kinondoni kwa kushirikiana na TCCIA kutoa elimu hiyo.
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:59 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Aidha ameonngeza kuwa wametumia semina, vipindi vya radio, vipeperushi na taasisi kuzungumza na taasisi mbali mbali kama NBAA, TCCIA na nyinginezo .
Amesema kuwa hii ni juhudi endelevu lakini kuna tatizo la watanzania kuwa na utamaduni wa kutokutaka kulipa kodi , naye mmoja wa wafanyabiashara waliogoma kufungua duka Kariakoo Bi. Saada Hussein alipozungumza na VOA ameeleza kuwa kugoma kwao kumetokana na bei kubwa ya mashine hizo ambazo wafanyabiashara wadogo na wakubwa ni vigumu kumiliki chombo hicho.
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:47 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Akijibu suala la kutokupenda kulipa kodi amesema wao wanalipa kodi kama kawaida na risiti wanazo na TRA wanawakagua kila wakati ila suala ni kwamba uamuzi wa TRA si sahihi kwasababu watu wenye mtaji wanatofautiana mashine ni shilingi laki 8 za Tanzania na wameambiwa watakatwa asilimia 10 ya mauzo yao kila mwezi ili kuweza kuilipia , ameongeza kuwa wana malipo ya kodi ya jengo, umeme, ulinzi na mwisho wa siku wanaona wananyonywa.
Kuhusu semina walizopewa na elimu anasema walielewa kuhusu bei za mashine lakini kwa sasa wameambiwa bei imepunguzwa hadi laki 6 lakini si wafanyabiashara wote wanaoweza kumudu kununua mashine hizo .
Kuhusu mgomo wao amesema huenda ukaisha bada ya siku tatu lakini alikuwa hajaelewa vizuri makubaliano yao mpaka atakapofika kazini siku inayofuata.
XS
SM
MD
LG