Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 08:43

Uchaguzi wa bunge Guinea wakosolewa.


Wapiga kura wakiwa kwenye mstari wakingoja kupiga kura zao septemba 28,2013 nchini Guinea.
Wapiga kura wakiwa kwenye mstari wakingoja kupiga kura zao septemba 28,2013 nchini Guinea.

Wafuatiliaji wa kimataifa wanaongeza wasiwasi kuhusu uchaguzi wa bunge wa mwezi uliopita nchini Guinea wakisema kuwa waligundua kasoro katika upigaji kura.

Wawakilishi kutoka Umoja wa Mataifa , Marekani, Ufaransa na Ecowas walisema katika taarifa ya pamoja Jumanne jioni suala hilo limesababisha baadhi ya kura kutozingatiwa hivyo kuzusha maswali katika matokeo ya kura.

Baadhi ya kura zilizotolewa wiki iliyopita zilionesha kuwa chama cha bwana Alpha Conde kinaongoza katika wiyala kadhaa.

Upinzani uliyakataa matokeo hayo ukisema kuwa uchaguzi uligubikwa na wizi mkubwa.

Bwana Conde alipuuzia shutuma Jumanne akisema zina ushawishi wa kisiasa na kusema kuwa hawezi kuruhusu kundi lolote kudhoofisha nchi.

Uchaguzi wa Septemba 28 ulitarajiwa kumaliza kipindi cha mpito ambacho kilianza kwa uchaguzi wa bwana Conde mwaka 2010. Uchaguzi uliahirishwa mara kadhaa katika kipindi cha miaka miwili kutokana na ghasia zilizokuwa zinaendelea nchini pamoja na vitisho vya kutokea ghasia zaidi kama uchaguzi ungeendelea.
XS
SM
MD
LG