Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 18:52

ICC yataka kukamatwa mwandishi habari Kenya.


Mwendesha mashataka mkuu wa ICC Fatou Bensouda.
Mwendesha mashataka mkuu wa ICC Fatou Bensouda.

Katika taarifa iliyorekodiwa Bensouda alisema Barasa alishiriki katika kuingilia mashahidi kwenye kesi inayomkabili naibu rais wa Kenya.

Mahakama ya uhalifu ya kimataifa imetoa kibali cha kukamatwa kwa mwandishi habari wa zamani anayeshutumiwa kwa kutoa hongo kwa mashahidi katika kesi ya naibu rais William Ruto .

Mwendesha mashtaka mkuu wa ICC Fatou Bensouda alitangaza jumane kwamba Kenya ilipata kibali cha kumkamata haraka Walter Barasa na kumpeleka katika mahakama ya ICC mjini Hague.

Katika taarifa iliyorekodiwa Bensouda alisema Barasa alishiriki katika kuingilia mashahidi kwenye kesi inayomkabili naibu rais wa Kenya.

Anasema ushahidi uliokusanywa hadi Sasa unaonesha kuna mtandao wa watu ambao wanajaribu kuvuruga kesi ya Ruto kwa kuingilia mashahidi upande wa mashtaka ambapo Barasa ni mmoja wao.

Amesema kutolewa kibali hicho cha kukamatwa itakuwa onyo kwa wengine. Kama atakutwa na hatia barasa anaweza kuhukumiwa kifungo cha miaka mitano jela.

Amri ya kukamatwa ilitolewa Jumatano wakati naibu rais Ruto anakwenda ICC kushiriki kuanza tena kusikilizwa kesi yake. Yeye na rais Uhuru Kenyatta wanashitakiwa katika kesi tofauti za uchochezi wa ghasia za mauaji baada ya uchaguzi wa rais mwaka 2007.
XS
SM
MD
LG