Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 19:13

Watu wafurika nje ya hospitali kumwona mwana mfalme.


watu wakisherehekea baada ya kutangazwa kuzaliwa mwana mfalme.
watu wakisherehekea baada ya kutangazwa kuzaliwa mwana mfalme.
Kundi kubwa la watu lilikusanyika nje ya hospitali mjini London likiwa na matumaini ya kumwona mtoto mwana mfalme aliyezaliwa .

Mwana mfalme William na mkewe Kate wanatarajiwa kuondoka katika jengo la hospitali hivyo kutoa nafasi kwa umma kumwona mtoto huyo mpya wa kifalme ambaye jina lake bado halijatangazwa. Wote Kate na mtoto wanaendelea vizuri.

Shambrashambra kubwa zilitawala Jumatatu kufuatia kuzaliwa kwa mtoto huyo ambapo Jumanne pia sherehe zilitarajiwa kupambwa na kupigwa mizinga ya heshima mjini London.

Mara baada ya kuzaliwa mwana mfalme waziri mkuu David Cameroon alisema Uingereza “iko katika wakati muhimu na kusema kuwa taifa lenye furaha linasherehekea”.
XS
SM
MD
LG