Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 27, 2023 Local time: 14:27

Ndege ya rais wa Somalia yapata hitilafu angani.


Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud akizungumza na waandishi wa habari.
Ndege ya rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud imetua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa Mogadishu jumatatu baada ya kuwa na matatizo kwenye injini.

Rais huyo hakujeruhiwa kwenye tukio hilo na hakukuwa na taarifa ya majeruhi yeyote.
Msemaji wa serikali Abdirahman Omar Osman alisema ndege hiyo iliondoka uwanja wa ndege wa Mogadishu saa tatu asubuhi lakini ilirudi mji mkuu baada ya kiasi cha dakika 20 za kukaa angani hitilafu ilitokea kwenye moja ya injini za ndege hiyo.

Afisa wa uwanja wa ndege aliiambia VOA kwamba ndege hiyo ilipata pancha wakati wa kutua Maafisa wa uwanja wa ndege wamekanusha taarifa za vyombo vya habari kwamba ndege hiyo ilishika moto.

Rais huyo na ujumbe wake walikuwa wakielekea Sudan Kusini kwa maadhimisho ya sherehe za uhuru wa nchi hiyo. Kundi hilo baadae lilipanda ndege nyingine na kuendelea na safari ya Sudan Kusini.
XS
SM
MD
LG