Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 08:34

Marekani yasheherekea uhuru wake.


Marekani inasheherekea Uhuru wake leo alhamisi. Tarehe 4 wanaadhimisha mwaka wa 237 wa uhuru kutoka utawala wa Waingereza. Raia wa Marekani kwa kawaida husheherekea kwa kuangalia magwaride , piknik, milipuko ya baruti, kucheza michezo mbali mbali na matamasha.

Mapambo ya siku ya Julai 4 siku ya Uhuru ni pamoja na rangi za bendera ya Marekani Nyekundu, nyeupe na Buluu.

Hapa Washington wanasheherekea kwa sherehe ya mwaka ya uhuru inayofanyika katika mnara wa taifa . Mwaka huu msanii atakayeongoza sherehe hizo ni Barry Manilow . Baruti zitapigwa baada ya tamasha hilo.

Andiko lilioandikwa na Thomas Jefferson mwezi Juni 1776 , tangazo la uhuru ni alama kuu inayothaminiwa kuliko zote ya uhuru. Baraza la congress lilipitisha rasmi andiko hilo wiki kadhaa baadaye ilipofika Julai 4.
XS
SM
MD
LG