Upatikanaji viungo

Bajeti ya nchi za Afrika Mashariki yasomwa.


Bunge la Tanzania Dodoma.
Mawaziri wa fedha wa mataifa manne ya afrika mashariki, kenya, Uganda, Tanzania na Rwanda wamesoma bajeti ya nchi zao kwa mwaka 2013 -2014.

Kwa sehemu kubwa nchi zote zinaongeza matumizi kwa ajili ya maendeleo ya nishati na miundo mbinu. Hata hivyo Uganda imepandisha bei ya mafuta na bidhaa muhimu jambo ambalo litaweza kuzusha malalamiko mapya nchini humo.

Serikali ya Kenya imetangaza bajeti yake chini ya mfumo mpya ya utawala na serikali ndogo zaidi. Mwandishi wetu wa Nairobi Mwai Gikonyo anasema hii ni mara ya kwanza kwa waziri wa fedha kusoma bajeti ambayo inazingatia zaidi maslahi ya wananchi walio wengi.


Kwa upande wa Tanzania mwandishi wetu Dina Chahali anasema bajeti itazingatia maeneo sita muhimu ya maendeleo ya nchi.

Bajeti ya Uganda inazingatia zaidi kuimarisha mipango ya nishati, miundo mbinu na mawasiliano kama anavyoeleza leylah Ndinda kutoka Kampala.

Na Rwanda serikali inajisifu kwa kufanikiwa kupunguza kutegemea msaada kutoka kwa wahisani kukamilisha mahitaji ya matumizi yake kwa mwaka na maendeleo ya nchi.

Mara baada ya kusomwa kwa bajeti hizo wananchi wamekuwa wakitoa maoni mbali mbali na tutakuleteni uchambuzi huo katika makala yetu ya Live talk katika matangazo ya jioni.
XS
SM
MD
LG