Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 22, 2024 Local time: 14:48

Viongozi wa Afrika Mashariki hawajaidhinisha sarafu ya pamoja


Viongozi wa Afrika Mashariki Kikwete, Kenyatta, Nkurunziza
Viongozi wa Afrika Mashariki Kikwete, Kenyatta, Nkurunziza
Viongozi wa nchi tano za Jumuiya ya Afrika Mashariki wamemaliza mkutano wao mkuu wa 11 nje kidogo ya jiji la Arusha bila ya kuchukua uwamuzi juu ya kutekelezwa makubaliano ya soko la pamoja na kuanzishwa kwa sarafu ya pamoja.

Viongozi hao wamerudisha ripoti na kuwataka mawaziri wao kutanzua masuala kadhaa yaliyobakia walokuwa nayo. Hata hivyo viongozi hao kutoka Tanzania Kenya Uganda Burundi na Rwanda wamesisitiza juu ya umuhimu wa kuimarisha mazingira ya biashara huru na uwekezaji katika jumuia yao.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:08 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Aidha wakuu hao wa nchi wamelitaka pia barza hilo kuendela na mchakato wa upanuzi wa utendaji wa mahakama ya afrika mashariki na kuja na majibu katika kikao kitakachofuata cha viongozi hao.

mwenyekiti wa sasa wa jumuiya ya afrika mashariki Rais wa Uganda Yoweri Moseven akizungumza katika mkutano huo alimkaribisha kwanza kiongozi mwenzake uhuru Kenyatta wa kenya akieleza matumaini ya kufanya kazi pamoja kwa maslahi ya wananchi wa afrika mashariki.

Kiongozi huyo wa muda mrefu wa Uganda amezitaka nchi wanachama kuimarisha mazingira ya uwekezaji ndani ya jumuiya na kuzialika nchi tajiri kuja kuwekeza katika jumuiya hiyo kutokana na utulivu uliyoko hivi sasa utajiri wa rasil mali na mazingira mazuri ya biashara.

"Wananchi wa Afrika Mashariki wanahamu kubwa hivi sasa kutoka kwenye umaskini na ukosefu wa maendeleo na kuchukua nafasi wanaostahiki ya maendeleo duniani"

Nae rais wa Kenya Uhuru Kenyata akizungumza kwa mara ya kwanza katika mkutano alisema kutokana na utajiri wa mafuta, gesi, madini na rasilmali nyenginezo ni lazima kufanya kazi pamoja kama jumuia moja na wala sio kila mtu kuendesha shughuli zake kama nchi pekee.

"Ni lazima kufanya kazi pamoja kuendeleza miradi ya miundo mbinu kuanzia bandari, barabara, reli na nishati kama miradi ya kikanda kuliko miradi ya nchi moja moja. Rrasilmali ya afrika mashariki na ya afrika kwa uijumla zinabidi kuwanufaisha waafrika na kuwatowa katika hali ya umaskini na kufikia jamii ya mapato ya wastani kama ilivyoahidiwa wakati wa uhuru."

Rais Kenyatta aliwataka viongozi wa afrika mashariki kusaidia katika kudumisha amani katika nchi jirani ya Somalia

"Inabidi kufanya kazi kwa pamoja kudumisha amani katika ukanda huu na kuhakikisha tunapambana na kutokomeza suala la ugaidi."
XS
SM
MD
LG