Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 31, 2024 Local time: 02:25

Mshukiwa wa mabomu ya Boston ahamishiwa jela.


Mshukiwa wa mabomu ya Boston Dzhokhar Tsarnaev akiwa kwenye gari ya wagonjwa.
Mshukiwa wa mabomu ya Boston Dzhokhar Tsarnaev akiwa kwenye gari ya wagonjwa.
Maafisa wa Marekani wanasema mshukiwa wa mabomu yaliyolipuliwa wakati wa Boston Marathon, Dzhokar Tsarnaev amehamishiwa kwenye kituo cha afya katika jela ya serikali kuu kutoka hospitali ambapo alikuwa akipata matibabu kwa majeraha aliyopata wakati alipokamatwa wiki iliyopita.

Idara ya usalama ya Marekani ilisema Ijumaa kwamba Tsarnaev alihamishiwa kwenye kituo cha afya cha serikali kuu cha Devens kwenye eneo la kituo cha jeshi huko Fort Devens, katika jimbo la Massachusets.

Msemaji hakutoa taarifa juu ya hali ya kijana huyo mwenye umri wa miaka 19, ambapo maafisa wamesema anapata matibabu ya jeraha lake la shingo. Idara ya magereza imesema eneo la Devens ni jela ambayo inatoa matibabu ya hali ya juu au ya muda mrefu kwa wafungwa.

Kaka wa mshukiwa na mshiriki katika ulipuaji mabomu,Tamela Tsarnaev alifariki katika mapigano na Polisi usiku wa alhamisi wiki iliyopita.

Maafisa wa New York wanasema washukiwa hao walikuwa wakipanga mashambulizi huko Times Square wakati wakikimbia maafisa. Mkuu wa Polisi wa New York Ray Kelly anasema Dzokhar aliwaambia wachunguzi walipanga waende New York ili kulipua milipuko yao iliyobaki.
XS
SM
MD
LG