Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 13:53

Rais Obama apongeza maendeleo ya kiuchumi Afrika.


Rais wa Marekani Barack Obama alipokutana na viongozi wa Afrika huko White House viongozi hao kutoka kushoto ni rais Macky Sall wa Senegal, rais Joyce Banda wa Malawi, Obama, rais Ernest Bai Koroma wa Sierra Leone na waziri mkuu wa Cape Verde Jose Maria Pereira.
Rais wa Marekani Barack Obama alikuwa mwenyeji wa viongozi wa Cape Verde, Malawi, Senegal na Sierra Leone katika White house alhamisi , akisifu hatua kubwa za uchumi nchi zao zimefanya pamoja na maendeleo ya kuimarisha utawala wa kidemokrasia.

Bw.Obama alisema kwamba wageni wake wote wa Afrika walikuwa na changamoto zao za kisiasa nyumbani, ikiwa ni pamoja na vita vya wenyewe kwa wenyewe Sierra Leone, mzozo wa hivi karibuni wa kikatiba huko Malawi na mzozo wa kisiasa huko senegal , hata hivyo nchi hizo zimefanikiwa kudumisha utulivu na kupata maendeleo ya kiuchumi.

Viongozi katika mkutano huo walikuwa ni Ernest Koroma wa SierraLeone , rais wa Senegal Macky Sall , waziri mkuu wa Cape Verde Jose Maria Pereira na rais wa Malawi Joyce Banda.
XS
SM
MD
LG