Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 07, 2024 Local time: 02:30

Raila Odinga kufungua kesi kumpinga Rais mteule Kenya.


Waziri mkuu Raila Odinga,
Waziri mkuu Raila Odinga,
Mahakama kuu nchini Kenya imesema iko tayari kusikiliza kesi itakayowakilishwa na waziri mkuu Raila Odinga kupinga hatua ya tume huru ya uchaguzi ya kumtangaza Uhuru Kenyatta kama mshindi wa kiti cha rais nchini humo.

Katika sherehe fupi iliyofanywa kwenye jengo la mahakama kuu mjini Nirobi jaji mkuu nchini Kenya DR. Willy Muntunga amesema mahakama kuu nchini Kenya iko tayari kusikiliza kesi hiyo ambapo majaji sita wamepewa jukumu la juu kuisikiliza kesi ya Raila Odinga itakayoendelea kwa muda wa siku 14 hii ikimaanisha kwamba sherehe za kuapishwa rais mpya itasubiri matokeo ya kesi hiyo itakayokuwa mahakamani.

Jaji mkuu anasema mahakama itatoa uamuzi wa haki bila upendeleo na katika muda uliowekwa kuambatana na katiba na sheria za Kenya.

Katika malalamiko yake waziri mkuu Raila Odinga anadai tume ya uchaguzi ya Kenya ilifanya makosa mengi wakati wa uchaguzi wa rais ikiwemo ya kiufundi, ambapo ameajiri mawakili kumi mashuhuri wa kumwakilisha kwenye kesi hiyo.

Habari zaidi zinasema kwamba waziri mkuu atawakilisha kesi hiyo mahakamani jumatano, na kwamba yuko tayari kuzingatia uamuzi wa mahakama.

Wakati huo huo serikali ya Kenya imempa ulinzi mkali Uhuru Kenyatta aliyeibuka mshindi wa uchaguzi mkuu uliofanyika Machi 4 mwaka huu.
XS
SM
MD
LG