Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 18:47

Majeshi Djibouti yapambana na waandamanaji .


Wanajeshi kwenye uwanja wa ndege huko Djibouti.
Wanajeshi kwenye uwanja wa ndege huko Djibouti.
Maafisa usalama huko Djibouti wamepambana na wapinzani waliokuwa wakipinga matokeo ya uchaguzi wa bunge wa Ijumaa.

Mapigano hayo yalianza Jumatatu baada ya wafuasi wa muungano wa upinzani Union of National Salvation (USN) walipojaribu kufanya maandamano ya kupinga kufuatia mkutano wa viongozi wa chama katika mji mkuu.

Mashahidi wanasema majeshi ya usalama yaliwakabili waandamanaji wakitumia virungu na gesi ya machozi katika jaribio la kuvunja maandamano hayo.
Maafisa wa serikali wanasema maandamano hayo yalikuwa kinyume cha sheria.
XS
SM
MD
LG