Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 23:19

Mauaji Sudan Kusini.


Watoto wakitembea katika maeneo ya watu waliopoteza makazi yao.
Watoto wakitembea katika maeneo ya watu waliopoteza makazi yao.
Gavana mmoja wa Sudan Kusini amesema Jumapili kwamba shambulizi la hivi karibuni la waasi lililolenga msafara wa familia limeuwa zaidi ya watu 100.
Gavana wa jimbo la Jonglei Kuol Manyang alisema maafisa wanaamini kabila la waasi wa Murle lilihusika na shambulizi la Ijumaa ambalo liliuwa watu 103, wengi wao wakiwa wanawake na watoto wakati kundi hilo lilipokuwa likihama na ng’ombe wake. Wengi bado hawajulikani walipo. Gavana Manyang alisema pia waasi wameripoti kuuwa wanajeshi 14 ambao walikuwa wakisindikiza msafara huo.
Hili ni shambulizi baya kuliko yote kuripotiwa katika jimbo la Jonglei tangu Umoja wa Mataifa kusema watu 900 waliuwawa huko 2011.
Maafisa walihusisha ghasia hizo na wizi wa ng’ombe na shambulizi hilo ilitokea miezi kadhaa baada ya Sudan Kusini kutangaza uhuru wake kutoka Sudan.
XS
SM
MD
LG