Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 31, 2024 Local time: 01:20

Rais Obama amelitaka bunge kuidhinisha haraka kiwango cha ukomo wa kukopa.


Rais Barack Obama akizungumza huko White house.
Rais Barack Obama akizungumza huko White house.
Rais wa Marekani Barack Obama amelitaka bunge kuidhinisha haraka kiwango cha ukomo wa kukopa cha Marekani na kusema anaunga mkono udhibiti wenye maana wa bunduki ili kujaribu kuzuia upigaji risasi wa watu wengi zaidi nchini Marekani.

Chini ya wiki moja kabla ya kuanza muhula wa pili Bw.Obama alisema katika mkutano na waandishi wa habari huko White house Jumatatu kwamba itakuwa kituko kwa wapinzani wake wa kisiasa kwenye bunge kufikiria kutokuongeza ukomo wa kukopa wa nchi wa kiasi cha dola trilioni 16.4 katika wiki zijazo.

Marekani imeshafikia ukomo wa kukopa lakini inazo fedha za kutosha kulipa madeni yake kwa wiki kadhaa. Rais anasema ukomo wa kukopa inabidi uongezwe si kwasababu matumizi ya serikali yanataka kuongezwa lakini ni kwa ajili ya Marekani kuweza kukidhi majukumu yake ya kifedha ambazo tayari imetumia.
XS
SM
MD
LG