Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 22:25

Mazishi ya waathiriwa wa shambulio la Newton yaanza


Gari la kubeba maiti likiwasili katika chumba cha kuhifadhia mwili katika maandalizi ya mazishi ya mtoto Jack Pinto mwenye umri wa miaka 6
Gari la kubeba maiti likiwasili katika chumba cha kuhifadhia mwili katika maandalizi ya mazishi ya mtoto Jack Pinto mwenye umri wa miaka 6
Mji wa Newton hapa Marekani unaanza kazi ngumu ya mazishi ya watoto 20 na watu wazima 6 waliouwawa katika mashambulizi ya bunduki kwenye shule ya msingi ya Sandy Hook huko katika jimbo la Connecticut.

Mazishi ya watoto wawili wa miaka 6 yatafanyika Jumatatu ya kwanza kwa wale waliopigwa risasi katika shule ya msingi ya Sandy Hook katika mji wa New town Connecticut. Watoto waliouwawa ijumaa walikuwa kati ya miaka 6 na 7.

Afisa wa Polisi alisema kwamba shule hiyo bado ni eneo la uhalifu na wapelelezi bado wanafanya kazi saa 24 kwa ajili ya kesi hiyo. Amesema watu wazima wawili walipigwa risasi lakini walinusurika kifo.

Rais Obama aliungana na waombolezaji huko New town Jumapili usiku , akiwaambia wale waliokusanyika kwenye ibada kuwa hawako peke yao kwenye kuomboleza na taifa limeachwa na maswali magumu.
XS
SM
MD
LG