Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 14, 2024 Local time: 23:29

Wanaharakati wa haki za binadamu Uganda wawasilisha ombi UN.


Ramani ya uganda
Ramani ya uganda

Desemba 10 ni siku ya kimataifa ya haki za binadamu, shirika lisilo la serikali la afya, haki za binadamu na maendeleo- CEHURD, likishirikiana na mashirika mengine 97 ya afya na kutetea haki za binadamu nchini Uganda na ulimwenguni kote, wamewasilisha ombi la dharura kwa kiongozi maalum wa umoja wa mataifa Bwana Anand Grover anayesimamia haki ya afya kwa wote, wakiiomba ofisi yake ichunguze madhara ya kiafya yatakayoletwa na mswada wa mashoga ikiwa utapitishwa na bunge la Uganda.

Kipengele kimoja kwenye mswada dhidi ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja kinasema iwapo utamjua mtu anayefanya mapenzi na mtu mwingine wa jinsia yake ni lazima umshitaki kabla ya masaa ishirini na manne kumalizika la sivyo utakamatwa na kushtakiwa.

Hii ni kumaanisha wewe kama mzazi ukijua mwanao anashiriki mapenzi ya jinsia moja ni lazima umshtaki. Ikiwa wewe ni daktari, mwito ni huo huo ingawa itakuwa kinyume na maadili ya udaktari wa kudumisha ubinafsi wa wagonjwa.

Sasa, wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wanahofia kuwa sheria hii ikipitishwa, basi madaktari wataogopa kuwahudumia mashoga, nao mashoga wataogopa kwenda kupata matibabu.

Ripoti iliyochapishwa mwaka huu ya utafiti uliofanya na shirika la Crane nchini Uganda inaonyesha kuwa visa vya uambukizwaji wa ukimwi miongoni mwa wanaume wanaofanya mapenzi na wanaume wenzao vimeongezeka kutoka asili mia 7 hadi asili mia kumi na tatu.

Ukifuatilia takwimu hizi maanani Jeff Ogwaro mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu anasema, Uganda ni nchi ambayo imetia bidii sana kuhakikisha kuwa inakomesha usambazaji wa ukimwi.

Serikali imegundua kuwa kuwabagua watu walio na virusi vya ukimwi inawafanya wagonjwa kuogopa kwenda kupata matibabu pamoja na ushauri kuhusu njia bora za kushiriki ngono. Kupitishwa kwa mswada huu kutawanyima wapenzi wa jinsia moja haki ya kupata matibabu. Hii ndio sababu tunawaomba waganda wawaambie viongozi wao bungeni kuwa hawaungi mkono mswada huu. Haki za binadamu ni haki za binadamu hata kama haziungwi mkono na wengi.

Baadhi ya viongozi wa kidini wamekuwa kwenye msitari wa mbele kuupigia debe mswada dhidi ya mashoga wakisema hauandamani na mafunzo ya vitabu vitukufu. Bunge linatarajiwa kuujadili mswada huu kabla ya kumalizika kwa mwaka huu
XS
SM
MD
LG