Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 09:13

SADC yajadili amani ya DRC, Zimbabwe, na Madagascar


Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe (kati), Rais Armando Guebuza wa msumbiji (2nd L red tie), Mfalme Mswati III wa Swaziland (L red and white tie) na RaisJoseph Kabila wa Congo (behind Guebuza) kwenye mkutano wa SADC
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe (kati), Rais Armando Guebuza wa msumbiji (2nd L red tie), Mfalme Mswati III wa Swaziland (L red and white tie) na RaisJoseph Kabila wa Congo (behind Guebuza) kwenye mkutano wa SADC
Jijini Dar es salaam , leo Asasi ya siasa, ulinzi na usalama ya jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika -TROIKA imefanya kikao cha kujadili masuala ya siasa na amani katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo - DRC, Zimbabwe na Madagascar ikiwa ni maandalizi ya mkutano wa dharura wa viongozi wa SADC.

Viongozi wa nchi wanachama wa SADC wanakutana jijini Dar es salaam Jumamosi katika kikao cha dharura kuzungumzia migogoro katika nchi hizo tatu za DRC, Zimbabwe na Madagascar .

Awamu ya kwanza ya kikao hicho cha TROIKA kilichokuwa chini ya uenyekiti wa Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete kilihudhuriwa pia na Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Jacob Zuma na Rais wa Namibia Hifikepunye Pohamba ambao ndio wanaounda asasi ya TROIKA.

Bernard Membe waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kiamtaifa wa Tanzania alipata nafasi ya kuzungumza na waandishi wa habari ikulu ya Dar es salaam Ijumaa ambapo kikao hicho cha awamu ya kwanza kilikuwa kinafanyika na kusema kuwa kazi kubwa ya TROIKA leo ni kuandaa agenda ya kikao hicho cha Jumamosi cha wakuu wa SADC.

Aidha kwa mujibu wa waziri wa mambo ya nje, awamu ya pili ya kikao hicho cha kuandaa agenda ya mkutano wa SADC wa kesho iliyoshirikisha wajumbe wengi zaidi imefanyika mchana wa leo jijini DSM na kuongozwa na Rais wa Msumbiji ambaye ndiye mwenyekiti wa SADC Armando Guebuza na kwamba kililitarajiwa pia kuhudhuriwa na Rais wa Uganda Yoweri Museveni.

Mgogoro ndani ya DRC ndio unatabiriwa utakuwa kiini kikubwa cha mazungumzo ya viongozi hao wa nchi 14 wanachama wa jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa AFRICA SADC, Jumamosi jijini Dar es salaam utakaojumuisha mapendekezo ya namna ya kufikia ufumbuzi wa mgogoro kati ya serikali ya nchi hiyo na waasi wa M23, mapendekezo yaliyotokana pia na kikao cha wakuu wa nchi za maziwa makuu kilichofanyika Kampala Uganda hivi karibuni.
XS
SM
MD
LG