Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 05:12

Ohio yashindaniwa vikali na Obama na Romney .


Wagombea wa kiti cha urais Marekani Barack Obama na Mitt Romney.
Wagombea wa kiti cha urais Marekani Barack Obama na Mitt Romney.
Uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2012 huwenda ukawa ni wa kihistoria kutokana na ushindani mkubwa ulojitokeza katika siku za mwisho za kampeni ya uchaguzi ambapo Rais Barack Obama yuko takriban sare na mpinzani wake Gavana Mitt Romney.

Kutokana na hali hiyo matokeo ya majimbo 7 yenye ushindani mkubwa ndiyo huwenda ikamua nani atakuwa rais mpya wa Marekani

Moja kati ya majimbo hayo ni Ohio maarufu kama “Buckeye state” ambalo litakuwa ni zawadi kubwa kwa yeyote atakayeshinsda. Jimbo hilo linawajumbe18 na inasemekana hakuna mgombea wa chama cha republican anayeweza kupata ushindi bila ya kushinda jimbo hilo..

Jimbo hilo lina umuhimu mkubwa kwa vile linawakazi wengi ambao kwa muda mrefu hawaungi mkono chama chechote cha kisiasa na hivyo uwamuzi wao unaweza kubadili hali ya mambo.

Mpaka sasa magazeti ya Ohio na baadhi ya kitaifa yanabashiri Ohio itachukua muda mrefu kutoa majibu ya kura wakati huo huo wakiongeza kwamba kuna uwezekano wa kura kuhesabiwa tena kutokana na malalamiko ambayo yameshafikishwa mahakamani kutokana na kasoro katika utaratibu wa upigaji kura. .

Immanuel Lyatuu, mkazi wa Columbus, Ohio anasema kila kambi inadai itapata ushindi na hali ni ya kusisimuwa katika jimbo hilo lililotembelewa mara nyingi kuliko jimbo jingine lolote lile na wagombea wa pande zote.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:26 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Anasema wakazi wengi wa jimbo hilo walikuwa wakitumiana ujumbe wa simu kuhudhuria mkutano wa mkutano wa Obama uliofanyika mkesha wa siku ya uchaguzi Romney alitembelea jimbo hilo siku ya uchaguzi ili kuwahamasisha wafuasi wao kupiga kura.
XS
SM
MD
LG