Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 12:00

Mabaki ya helikopta ya Uganda yapatikana Kenya


Chris Kasaija, afisa wa cheo cha juu wa jeshi la anga la Uganda aokolewa mjini Nanyuki
Chris Kasaija, afisa wa cheo cha juu wa jeshi la anga la Uganda aokolewa mjini Nanyuki

Juhudi za kuwatatuta wanajeshi saba wa Uganda wanaodhaniwa wamenusurika na ajali ya helikopta ziliendelea Jumanne huko mlima Kenya

Timu za waokozi Kenya wanasema wamepata miili ya wanajeshi wawili wa Uganda walofariki katika ajali ya helikopta ya jeshi la Uganda karibu na Mlima Kenya Jumapili usiku.

Simon Gitau, naibu mkuu katika idara ya mbuga ya kitaifa ya Mt. Kenya amesema timu ya waokozi ilipata maiti mbili nje ya helikopta hiyo ambayo ilikuwa bado inaungua moto Jumanne na kwamba kuna uwezekano wa kupata maiti nyingine ndani ya helikopta hiyo.

Akizungumza na Sauti ya Amerika msemaji wa wizara ya Ulinzi nchini Kenya Bogita Ongeri, anasema wameshapata helikopta zote tatu zilizoanguka wamezipata, na juhudi zinaendelea kuwatafuta wanajeshi watano ambao hawajajulikana walipo.

please wait

No media source currently available

0:00 0:04:06 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

.

Alisema wanajeshi wengine watano waliokuwa kwenye helikopta nyingine ya jeshi la Uganda wamepatikana wakiwa hai. Maafisa wanasema wapelelezi wanadhani kuwa hali mbaya ya hewa ndiyo iliyosababisha ajali za helikopta nne za jeshi la Uganda huko Kenya.

Helikopta hizo zilikuwa njiani kuungana na kikosi cha walinda amani wa Umoja wa Afrika kwa mapigano dhidi ya wanamgambo wa al-Shabab nchini Somalia . Helikopta moja ilitua salama katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa Kenya.
XS
SM
MD
LG