Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 11:19

Viongozi wa Afrika hawajakubaliana juu ya Congo


Viongozi wa mataifa ya kanda ya Maziwa Makuu wakutana Kampala
Viongozi wa mataifa ya kanda ya Maziwa Makuu wakutana Kampala
Viongozi walitangaza Jumatano baada ya kukutana Kampala kwamba wameweza kukubaliana juu ya haja ya kupaleka kikosi cha kimataifa kupambana na makundi ya waasi huko mashariki ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.

Hata hivyo, katika taarifa yao ya mwisho viongozi hao hawakutaja kutokubaliana kwao juu ya namna ya kuundwa kwa kikosi hicho ingawa wameeleza haja ya kuushinda uwasi huo kwa haraka iwezekanavyo.
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:00 0:00
Kiungo cha moja kwa moja


Rais wa Uganda Yowerei Museveni alisema viongozi hao wamekubaliana kukutana katika muda wa mwezi mmoja unaokuja baada ya mawaziri wa ulinzi wa mataifa manane kukutana na kutayarisha mipango yote ya kuundwa kwa kikosi hicho katika muda wa wiki mbili zijazo.

Tofauti kubwa iliyojitokeza kwenye mkutano huo ni msimamo inayotofautiana kati ya Kongo na Rwanda.Serikali ya Kinshasa inapenmdelea kuwepo na kikosi cha kimataifa kisichopendelea upande wowote kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili, huku Kigali inapendelea kikosi cha kikanda, kipelekwe ndani ya Jimbo la Kivu.

Wimbi la ghasia nchini DRC lilianza Aprili, wakati wanajeshi kutoka jeshi la taifa kuasi na kuunda kundi la waasi la M23. Tangu wakati huo, mapigano katika jimbo la Kivu ya Kaskazini yamesababisha maelfu ya watu kukimbilia mpakani na kuingia nchi jirani ya Uganda.
Katika mkutano na waandishi wa habari Afrika Kusini Jumanne, waziri wa mambo ya nchi ya nje Marekani, Bi Clinton alitoa wito kwa viongozi kanda hiyo ya wa Maziwa Makuu, kufanya kazi pamoja kukomesha vurugu katika mashariki ya Kongo.

“Uamuzi wa Uganda Rwanda na DRC kuanza tena mazungumzo ni hatua muhimu. Kumekuwa na ongezeko la ghasia, ubakaji, mauaji, na ukiukaji mbaya wa haki za binadamu katika kipindi cha miaka kadhaa iliyopita iliyokuwa inafanywa na makundi ya wahuni na waasi. Na tunaunga mkono juhudi za DRC na tunazihimiza nchi zote katika kanda hiyo ikiwa ni pamoja na Rwanda kufanya kazi pamoja ili kukata msaada kwa waasi wa M23 na kuwanyanganya silaha na kuwafikisha mahakamani viongozi wao.”

Wote marais wa Kongo Joseph Kabila na Paul Kagame wa Rwanda walihudhuria mkutano wa Kampala, ambao ulikuwa na lengo la kupunguza mvutano kati ya nchi hizo mbili.

Baada ya mkutano huo, waziri wa mambo ya nchi za kigeni wa Uganda Oryem Okello aliwambia waandishi habari kwamba makubaliano hayo ni ishara kwamba marais Kabila na Kagame wako tayari kushirikiana.
XS
SM
MD
LG