Watu watatu wamekufa kufuatia jengo kuanguka huko India

Hii sio mara ya kwanza majengo kuanguka nchini India. June 10, 2021. (AP Photo/Rafiq Maqbool)

Gazeti la India Today linaripoti kuwa mtu mmoja aliokolewa Jumapili, karibu saa 18 baada ya jengo kuanguka

Maafisa wa India wanasema watu wasiopungua watatu waliuawa na wengine 10 kujeruhiwa nchini India wakati jengo lilipoanguka Jumamosi huko Bhiwandi.

Gazeti la India Today linaripoti kuwa mtu mmoja aliokolewa Jumapili, karibu saa 18 baada ya jengo kuanguka.

Shughuli za uokoaji zilikuwa zikiendelea kuwatafuta watu wengine ambao huenda wamekwama chini ya kifusi, kulingana na mamlaka.