Washukiwa wa shambulizi la Mpeketoni waachiwa huru

Mashambulizi ya ugaidi yamekuwa yakitokea mara kwa mara nchini Kenya.

Mahakama ya juu huko Mombasa nchini kenya iliwaachia huru washukiwa wa shambulizi la ugaidi mfanyabiashara kutoka Malindi, Mahadi Swaleh mahadi pamoja na mwenzake Dyana Salim Suleiman.

Washukiwa hawa walihusishwa katika shambulizi lililotokea Mpeketoni mwezi Juni mwaka 2014 na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 60 na majeruhi kadhaa.

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa kutoka Kenya, Kasuja Onyanyi alisema kwamba hatua iliyofikiwa na mahakama nchini kenya ni pigo kubwa sana kwa vyombo vya usalama wa nchi kupigana na ugaidi kwa sababu wengi wa wakenya hawatakuwa na Imani na maamuzi ya mahakama.

Your browser doesn’t support HTML5

Mahojiano ya VOA na Kasuja Onyonyi