Wananchi Zanzibar wana matumaini na serikali mpya

Wananchi Zanzibar wana matumaini na serikali mpya

Wananchi visiwani Zanzibar wanaeleza matumaini yao na kuridhika na ahadi zilizotolewa na makamu wa kwanza wa rais Maalim Seif Sharif Hamad ya kudumisha ushirikiano kati ya viongozi, utendaji kazi na kujenga Zanzibar mpya.

Seif Sharif alitoa ahadi hizo akiwa pamoja na baadhi ya mawaziri wa serikali mpya ya Zanzibar katika hotuba kwenye mkutano wa hadhara huko Kibanda Maiti.

Wakizungumza na Sauti ya Amerika baadhi ya wananchi wameeleza kufuruhishwa na matamko ya waziri wa biashara ya kupambana na vyakula vibovu Zanzibar akisema haitokubali mambo hayo kutokea tena.

Wamesema wanafikiri maendeleo ya kweli yatapatikana kwasababu ya ukweli wa viongozi wapya na kwa upande wa elimu wanasema hawajui kitakacho tendeka lakini wana matumaini.

Kuhusiana na afya wananchi hao walisema inaonekana mwelekeo umekuwa mzuri hasa baada ya kuthibitishiwa na waziri wa Afya kwamba tatizo la madawa litatanzuliwa haraka.