Naibu waziri Waititu awekwa rumande Kenya

Ferdinad Waituti naibu waziri wa maji wa Kenya

Rais Mwai Kibaki wa Kenya na Waziri Mkuu wake Raila Odinga wamemsimamisha kazi Waititu kwa muda ili kutoa nafasi ya kufanyika uchunguzi huru
Naibu waziri wa maji katika serikali ya Kenya, Ferdinand Waititu aliyetoa matamshi ya chuki na uchochezi nchini humo, amefikishwa katika mahakama moja mjini Nairobi alhamisi, na amewekwa rumande ambapo mahakama itaamua iwapo ataachiwa huru kwa dhamana.

Bwana Waititu alisema kuwa hakukusudia kusema hivyo wakati alipokuwa akiwahutubia watu kwenye eneo lake ni kwamba ulimi wake uliteleza.

Your browser doesn’t support HTML5

Ripoti ya Mwai Gikonyo, Nairobi


Kenya imekumbwa na ghasia za kikabila hivi karibuni wakati ikielekea kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Machi mwakani.

Baadhi ya wananchi nchini humo wanahisi kuwa uchaguzi mkuu ujao utakuwa na ghasia kama zile zilizotokea mwaka 2007 ambazo zilisababisha vifo vya zaidi ya watu 1,000 na wengine wengi kukoseshwa makazi na kuwa wakimbizi ndani ya nchi yao.