Waislam watumia fursa ya sherehe za Eid kuzileta jamii za waliowachache pamoja

Your browser doesn’t support HTML5

Baraza la uhusiano wa Kiislam na Marekani limetumia fursa ya sherehe za Idd el Fitr 2022 Marekani kuondoa wasiwasi kutokana na kuripotiwa ongezeko la matukio ya chuki dhidi Waislam nchini Marekani.

Baraza linafanya juhudi ya kuzileta pamoja jamii za waliowachache kuondoa wasiwasi huo ambapo sherehe ya kumalizika kwa mfungo wa Ramadhani, Eid el Fitr ni fursa ya kukabiliana na changamoto hiyo.