Wadau wa mazingira wadadisi usalama wa nguo za mitumba kwa mazingira

Your browser doesn’t support HTML5

Wanamazingira wadai kuwa nguo za mitumba zinachangia kuongeza tatizo la taka na baadhi ya watu wanahoji iwapo nchi za Magharibi na Asia zinazo safirisha mitumba kwenda nchi za Afrika wanatumia fursa hiyo kugeuza bara hilo ni jaa la kutupa uchafu.

Wanadai kuwa baadhi ya nguo ambazo huwasili haziwezi kutumika. Lakini kwa upande wa wauzaji mitumba wanasema hawajui wangefanya nini kama hii biashara isingekuwepo na wakazi wengine wa Kenya wanasema wananufaika na nguo hizo zilizochakaa.